Msimamizi wa Watoto Baraza la Watoto mkoani Mwanza, Karus Masinde, akizungumza na BMG.
Na George Binagi-GB Pazzo
Baraza la Watoto mkoani Mwanza, umetoa rai kwa wanajamii kuepuka vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa watoto kwani vitendo hivyo husababisha watoto kutofikia malengo yao maishani.
Hivi karibuni msimamizi wa baraza hilo ambalo liko chini ya shirika la Mwanza Youth and Children Networ (MYCN), Karus Masinde, aliiambia BMG kwamba ukatili wa watoto ikiwemo ukatili wa kingono na vipigo husababisha watoto wengi kuyakimbia makazi yao na hivyo mwelekeo wa maisha yao pia kutoweka.
"Jamii ambazo bado zina mila za kuonesha ukatili kwa watoto ziachane nazo kwa sababu zinatia changamoto kubwa, watoto wanashindwa kutimiza malengo yao kutokana na ukatili wa kimwili, kingono na kisaikolojia miongoni mwa changamoto nyingi". Alibainisha Masinde.
James John ni mmoja wa wanafunzi wa darasa la tano kutoka shule ya msingi Kitangiri A Jijini Mwanza, mwenye ndoto za kuwa Rais kwa lengo la kupambana na ukatili hususani kwa wasichana na wanawake nchini.
"Mimi ndoto zangu nataka kuwa Rais, na mambo ambayo naona hayako sawa ni ukatili ikiwemo ubakaji ambayo nitapambana nayo ikiwa ndoto yangu itatimia". Anadokeza John.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni