Mchezaji asiyetakiwa Manchester
United, Bastian Schweinsteiger, ameshinda tuzo maalum nchini
Ujerumani ijulikanayo kama BAMBI.
Licha ya kucheza michezo michache na
Manchester United mwaka jana Waandaaji wa Tuzo hizo za Vyombo vya
Habari wametunuku tuzo Schweinsteiger kwa mchango wake katika michezo
ya kimataifa.
Schweinsteiger, 32, alistaafu
kucheza soka kimataifa mwezi Agosti, akiwa ametwaa kombe la dunia na
kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Euro.
Kocha wa Ujerumani Joachim Low naye alitwaa tuzo ya Bambi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni