Binti wa miaka 14 amekuwa Muingereza
wa kwanza kuridhia mwili wake kuhifadhiwa katika mitungi maalum ya
kungandisha mwili, baada ya kushinda kesi ya pingamizi lililowekwa na
baba yake.
Binti huyo ambaye ni mkazi wa
London, alibainika kuwa na saratani Agosti mwaka jana na kisha kufa
mwezi mmoja uliopita baada ya tiba zote alizopatiwa kushindwa
kumtibu.
Binti huyo alivutiwa na ahadi ya
kwenye tovuti ya kampuni ya cryogenic, ambayo ilimshawishi iwapo
mwili wake utagandishwa kwenye mitungi yao, siku moja itakapopatikana
tiba atapa fursa ya kutibiwa na kufufuka.
Barua ya binti huyo iliyoeleza sababu ya yeye kutaka mwili wake ugandishwe kwenye mitungi ili ikipatikana tiba atibiwe na kufufuka
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni