Bondia David Haye na Tony Bellew
wametia saini makubaliano ya kupigana katika pambano la ngumi la
uzito wa dunia Jijini London mwakani.
Mabondia hao watapanda ulingoni
katika dimba la 02 Machi 4 mwakani baada Bellew bingwa wa dunia uzito
wa cruiserweight, kujipandisha daraja ili apambane katika uzito wa
juu.
Bellew alisisitiza kuwa anataka
kupambana na bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu, tangu ashinde
mkanda wa WBC cruiserweight katika majira ya joto.
Tony Belew akimdunda BJ Flores katika pambano la uzito wa cruiserweight
David Haye akimdunda Arnold Gjergjaj baada ya kurejea tena ulingoni mwezi Mei
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni