Goli la kusawazisha la David Silva
limeihakikishia Manchester City kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya kwa mwaka wa nne mfululizo baada ya sare ya 1-1 na
Borussia Monchengladbach.
Katika mchezo huo Manchester City
ilijikuta ikiwa nyuma baada ya Raffael kuachia shuti kali la umbali
wa yadi 15 lililompita kipa Claudio Bravo na kutinga wavuni.
Hata hivyo goli hilo lilisawazishwa
na David Silva kwa goli alilolifunga kwa kuteleza na kuutumbukiza
mpira wavuni akiunganisha krosi ya chini ya Kevin de Bruyne.
Shuti lililopigwa na Raffael likitinga wavuni baada ya kushinda kipa Bravo
Mpira uliopigwa na David Silva ukitinga wavuni na kusawazisha goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni