Timu ya Celtic imeondolewa katika
Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Barcelona ikiongoza kundi C katika
michuano hiyo.
Katika mchezo huo Lionel Messi
alifunga goli la kwanza kufuatia pasi ya kiufundi kutoka kwa
Neymar, na kisha baadaye kipa Craig Gordon akamnyima goli Luis
Suarez.
Mchezaji Celtic Moussa Dembele
alijikuta akipoteza nafasi nzuri ya kufunga kabla ya Lionel Messi
kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penati.
Lionel Messi akiachia shuti la mguu wake wa kushoto na kuandika goli la kwanza
Lionel Messi akifunga goli la pili kwa mkwaju wa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni