Timu ya Arsenal imeshindwa kukwea na
kuongoza kundia A katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutoka sare
ya goli 1-1 na Paris St-Germain katika dimba la Emirates.
Ilionekana kama Arsenal wataweza
kuongoza kundi hilo licha ya kufungwa goli la mapema lililofungwa kwa
kuteleza na Edinson Cavani akiunganisha krosi ya Blaise Matuidi.
Olivier Giroud alifunga kwa mkwaju
wa penati na kusawazisha goli, na kisha baadaye Marco Verratti
akajifunga, kabla ya Alex Iwobi naye kujifunga kwa mpira wa kichwa
uliopigwa na Lucas Moura.
Edinson Cavani akiteleza na kufunga goli la kwanza katika mchezo huo
Alex Iwobi akiwa anashangaa baada ya kujifunga huku kipa wao akiwa amelala chini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni