Donald Trump amesema yeye ni muumini
wa kutetea uhai, hivyo basi wanawake wajawazito wanaotaka kutoa mimba
watalazimika kusafiri kwenda kwenye majimbo yenye sheria inayoruhusu
utoaji mimba kwa kuwa hatohalalisha utoaji mimba kwenye majimbo yote.
Akiongea kwenye mahojiano na kituo
cha CBS, amesema atamchagua Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ambaye naye ni
muumini wa kutetea uhai, ili kuhakikisha mahakama hiyo ya juu nchini
Marekani hairuhusu sheria za utoaji mimba.
Katika mahojiano hayo yaliyorushwa
jumapili, Trump amethibitisha nia yake ya kujenga ukuta katika mpaka
na Mexico, ingawa amekiri katika baadhi ya maeneo ataweka fensi, na
kuahidi kuwarejesha kwao wahamiaji milioni 2 ama milioi 3 wenye
rekodi za uhalifu.
Donald Trump akifanya mahojiano kwenye jumba lake la kifahari
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni