Mchezaji wa Manchester United,
Memphis Depay, amefunga mara mbili wakati Uholanzi ikiifunga
Luxembourg magoli 3-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga
michuano ya kombe la dunia 2018.
Depay, aliyesainiwa na Manchester
United kwa paundi milioni 25 akitokea PSV mwaka 2015, amecheza dakika
20 akiwa na Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza katika
msimu huu.
Lakini akitokea benchi Depay
alifunga goli lake la kwanza kwa mpira wa kichwa na kwa shuti la
mpira wa adhabu, huku Arjen Robben akiwapa Wadachi hao goli la
kuongoza lililozawazishwa na Maxime Chanot.
Arjen Robben akiachia shuti lililozaa goli la kwanza la Uholanzi
Memphis Depay akishangilia baada ya kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni