.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 24 Novemba 2016

ESRF YASHIRIKIANA NA GETENERGY KUANDAA MKUTANO WA AFRIKA WA MAFUTA NA GESI

Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) imeshirikiana na kampuni ya Getenrgy kuandaa mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi (GETENERGY VTEC AFRICA 2016) ambao unafanyika nchini kwa siku tatu kuanzia Novemba, 21-23, 2016.

Katika hotuba yake ya utangulizi, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kuwa mkutano huo umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta na gesi kutoka nchi mbalimbali Afrika ikiwepo serikali, viwanda, mashirika ya maendeleo na vyuo ambavyo vinatoa elimu ya mafuta na gesi.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akitoa neno la utangulizi katika Mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi.

“Malengo ya mkutano huu ni kuangalia changamoto gani ambazo zinalikabili Bara la Afrika katika sekta ya mafuta na gesi, kubadilisha ujuzi kwa wataalamu wa mataifa ambayo yameshiriki na kujadili hatua ya kuchukua ili kuboresha sekta hii lakini pia utasaidia kukuza ushirikiano baina ya nchi washiriki,

“Katika mkutano washiriki wataisaidia Serikali na wadau kuweka mikakati ya kutekeleza na yenye ufanisi kuhusu sekta ya mafuta na gesi na kama Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamiii tutaendelea kushirikiana na wadau kutafuta changamoto zinazokabili sekta na mbinu za kutumia ili kuyatatua,” alisema Dkt. Kida.
Mgeni rasmi katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu akizungumza umuhimu wa mkutano huo na jinsi ambavyo unaweza kuwanufaisha Watanzania.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu alisema, Serikali kwa sasa inataka kuhakikisha kunakuwapo na wataalamu wengi ili kunapokuwepo na sehemu ambazo kunapatikana mafuta au gesi waweze kushiriki wenyewe ili kipato kinachopatikana kiwanufaishe wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Nchi ina akiba nyingi ya gesi na tunategemea kupata mafuta baadae lakini tunangaalia upande wa wataalamu, tunahitaji kuwa na wataalamu katika sekta ya mafuta na gesi ili tutakapoanza shughuli ya uchimbaji tayari tuwe na wataalamu wanaohitajika hapa nchini,

“Huu ndiyo mchango wa ndani, hatuwezi kufanya sisi pekee lazima tuwe na wageni lakini pia tuwe na Watanzania wanaotumikia sekta hii na wanaofaidika na uchimbaji wa hayo mafuta,” alisema Mama Samia.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akieleza jinsi ambavyo Serikali imejipanga kuinua sekta na mafuta na gesi ili Watanzania wengi wanufaike na uwepo wa mafuta na gesi nchini.

Nae Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisema Serikali imejipanga kuboresha sekta ya mafuta na gesi kwa kutoa elimu kuhusu sekta hiyo katika baadhi ya vyuo mbalimbali nchini ili wahitimu wanapomaliza waweze kuingia moja kwa moja katika sekta hii.

“Tupo katika orodha ya nchi 20 Afrika ambazo zinafanya vizuri, baada ya miaka mitano tutakuwa tumepiga hatua na mtaona ni jinsi gani tumefanikiwa, kwasasa tuna wanafunzi wamehitimu UDOM na tunashirikiana na China na Uingereza kwahiyo niwahakikishie kuwa tumejipanga,” alisema Prof. Muhongo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Getenergy, Virginia Baker akitoa taarifa kuhusu kampuni hiyo, malengo na umuhimu wa kufanyika kwa mikutano hiyo.

Mikutano ya GETENERGY VTEC kwa mwaka 2016 tayari imeshafanyika katika nchi ya Mexico na Uingereza na imekuwa ikikutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta na gesi ili kujadili jinsi sekta hiyo inaweza kuboreshwa na kuwa bora zaidi kuliko ilivyo sasa.
Wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta na gesi kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mkutano wa mafuta na gesi ambao mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu.
 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu akipewa maelekezo kutoka kwa msimamizi wa banda la Chuo cha AGR TRACS kuhusu masomo yanayotolewa na chuo hicho. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni