.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 26 Novemba 2016

FIDEL CASTRO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa rais wa Cuba, Fidel Castro amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90. 

Castro aliyekuwa na msimamo mkali, aliiongoza Cuba kwa miaka mingi kabla ya kukabidhi madaraka kwa kaka yake Raul mwaka 2008. 

Fidel Castro alizaliwa mwaka 1926 kusini magharibi kwa jimbo la Oriente. 

Katika maisha yake ya harakati alijikuta akikamatwa na kufungwa mwaka 1953 kabla ya kuachiwa mwaka 1955. 

Alichaguliwa kuwa rais wa Cuba mwaka 1976 hadi mwaka 2008 alipokabidhi uongozi kwa kaka yake baada ya kusumbuliwa na maradhi mara kwa mara.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni