Bi. Hillary Clinton amesema
kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais Marekani, kumechangiwa na
Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI).
Bi. Clinton amesema kauli ya
Mkurugenzi wa FBI James Comey kuwa wameanzisha uchunguzi mpya dhidi
ya tuhuma za kutumia seva ya barua pepe binafsi akiwa Waziri wa Mambo
ya Nje ilimpunguzia kasi ya ushindi.
Kauli hiyo ya mgombea huyo wa urais
wa chama cha Democratic imenaswa katika maongezi yake kwa njia ya
simu na wafadhili wakuu wa chama cha Democratic, na kuvujishwa kwenye
vyombo vya habari.
Mkurugenzi wa FBI James Comey
Wakati huo huo maandamano
yanaendelea kupinga ushindi wa Dodald Trump katika miji kadhaa ya
Marekani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni