Mchezo wa nne wa kocha Gareth
Southgate tangu apewe fursa ya kusaidia kuinoa Uingereza umeishia kwa
sare ya aibu ya magoli 2-2 dhidi Hispania waliofunga mara mbili
katika dakika za mwisho kwenye mchezo wa kirafiki katika dimba la
Wembley.
Uingereza inayoonekana kuimarika
tangu Southgate atwae mikoba ya Sam Allardyce walianza kufunga goli
la kwanza kupitia kwa Adam Lallana kwa mkwaju wa penati ya mapema
iliyotolewa baada ya kipa wa Hispania Pepe Reina kumuangusha Jamie
Vardy.
Jamie Vardy aliongeza goli la pili
akipiga kichwa cha chini cha kuchupa akiunganisha mpira wa krosi ya
Jordan Henderson katika kipindi cha pili. Hispania ilisawazisha
kupitia kwa Iago Aspas dakika ya 90 na Isco kufunga la pili dakika za
nyongeza.
Isco akifunga goli la kusawazisha kwa mpira uliompita tobo kipa wa Uingereza
Jamie Vardy akiruka kichwa cha kuchupa chini na kufunga goli
Kipa Pepe Reina akimuangusha mshambuliaji Jamie Vardy
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni