Alexis Sanchez ameondoa hofu ya kuwa
majeruhi katika mchezo wa Arsenal dhidi ya Manchester United baada
ya kufunga magoli mawili wakati Chile ikiifunga Uruguay magoli 3-1
katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia.
Nyota huyo wa Arsenal alifunga
magoli hayo mawili katika kipindi cha pili na kuipatia Chile pointi
tatu muhimu. Katika mchezo huo Edinson Cavani aliifungia Uruguay goli
la kuongoza baada ya dakika 14 lakini likasawazishwa na Eduardo
Vargas.
Mshambuliaji Edinson Cavani akishangilia goli alilofunga
Alexis Sanchez akishangilia moja ya magoli aliyoyafunga jana usiku
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni