Mchezaji nyota Lionel Messi amefunga
moja na kusaidia mengine mawili wakati Argentina ikicharuka katika
mchezo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia dhidi ya
Colombia jana usiku.
Nyota huyo wa Barcelona aliifanya
Argentina ipate goli la kwanza kwa mpira wa adhabu alioupiga katika
dakika ya 10, kabla ya kutengeneza mengine kwa Lucas Pratto na Angel
di Maria katika kipindi cha pili.
Ushindi huo wa Argentina umeondoa
machungu ya kufungwa magoli 3-0 na Brazil wiki iliyopita, na kufufua
matumaini yao ya kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia 2018
itakayofanyika nchini Urusi.
Kipa David Ospina akiruka bila ya mafanikio kuufuata mpira uliopigwa na Lionel Messi
Lucas Pratto akiwa ameachia shuti lililojaa wavuni baada ya kupata pande kutoka kwa Messi
Angel
di Maria akiwa ametikisa nyavu baada ya Messi kupasua ngome na kumpatia pasi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni