Italia imepata ushindi wa magoli 4-0
katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia dhidi ya
Liechtenstein, lakini Hispania imeendelea kuongoza kundi lao la G kwa
tofauti ya magoli baada ya kuifunga Macedonia magoli 4-0.
Katika mchezo huo Hispania ilipata
goli la kwanza baada ya Darko Velkoski kujifunga na kuongeza la pili
kupitia Vitolo, na kisha Nacho Monreal kuongeza la tatu kabla ya
Aritz Aduriz kukamilisha ushindi huo kwa kufunga goli la nne.
Katika mchezo wa Italia magoli
yalifungwa kabla ya kipindi cha pili ambapo Andrea Belotti alitikisa
nyavu mara mbili huku nao Ciro Immobile pamoja na Antonio Candreva
wakifunga goli moja kila mmoja. Katika mchezo mwingine wa kudi G
Israel 3-0 Albania.
Andrea Belotti akiachia shuti lililompita tobo golikipa na kujaa wavuni
Andrea Belotti jana usiku alikuwa hazuiliki hapa akipachika goli lake la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni