Matumaini ya Wales kufuzu michuano
ya kombe la dunia 2018 yamepata pigo kubwa baada ya goli la dakika
za mwisho la Aleksandar Mitrovic kuisawazishia Serbia na kuwanyima
ushindi katika dimba la Cardiff.
Licha ya wageni Serbia kuanza kwa
kasi katika mchezo huo, Gareth Bale aliifanya Wales kupata goli la
kuongoza baada ya Hal Robson-Kanu aliyecheza bila ya kuchoka kumfanya
Matija Nastasic kufanya kosa lililozaa goli.
Mshambuliaji nyota wa Wales Gareth Bale akiachia shuti lililojaa wavuni
Mpira wa kichwa uliopigwa na Aleksandar Mitrovic ukielekea kuja wavuni
Gareth Bale nusura afunge goli la pili katika mchezo huo ulioishia kwa sare ya 1-1
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni