Jaji mmoja huko Atlanta amemuagiza
mpenzi wa marehemu Bobbi Kristina Brown, Nick Gordon, kulipa kiasi
cha dola za Marekani milioni 36 kwa kusababisha kifo chake kimakosa.
Kristina Brown, ambaye ni binti wa
Whitney Houston na Bobby Brown, alikutwa akiwa amepoteza fahamu
kwenye bafu, uso wake ukiwa kwenye maji Januari 2015.
Mpenzi wake Gordon, ambaye alikuwa
akiishi naye pamoja na rafiki moja walikuwa katika ripoti ya polisi
iliyoeleza walikuwemo nyumbani wakati wachunguzi walipofika katika
eneo la tukio la kifo.
Bobby Brown akionyesha picha ya utoto ya Bobbi Kritina wakati akitoa ushahidi Mahakamani
Bobby Brown akiwa kwenye majonzi makali wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni