Kocha Jose Mourinho ametolewa nje
kwa mara ya pili ndani ya mwezi moja wakati Manchester United ikitoka
sare ya goli 1-1 na West Ham katika dimba la Old Trafford.
Kocha huyo Mreno alipiga teke chupa
ya maji, katika kukerwa na uamuzi wa refa Jon Moss kumuonyesha kadi
ya njano Paul Pogba kwa kujirusha.
Katika mchezo huo Manchester United
ilijikuta ikifungwa dakika ya pili tu ya mchezo na Diafra Sakho
akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Dimitri Payet.
Zlatan Ibrahimovic alisawazisha goli
hilo katika dakika ya 21 kwa kuupiga kichwa mpira uliopingwa na Paul
Pogba.
Kipa David De Gea akiangalia wavuni mpira uliopigwa na Diafra Sakho
Zlatan Ibrahimovic akiruka juu na kuupiga mpira kichwa uliosawazisha goli
Guu la Zlatan Ibrahimovic likiwa juu na kuhatarisha usalama wa wachezaji wa West Ham
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni