Timu ya Barcelona itaingia wiki
ijayo katika mchezo wa kwanza wa El Clasico katika msimu huu wakiwa
pointi sita nyuma ya Real Madrid baada ya kutoka sare Real Sociedad.
Mabingwa hao ambao wameshindwa
kupata ushindi katika dimba la Anoeta katika michezo yake minane,
ilibidi wapambane kiume kusawazisha goli ili kuambulia pointi moja.
Alikuwa Willian Jose aliyewapatia
wenyeji goli la kwanza katika mchezo huo, huku Gerard Pique akisaidia
kuutumbukiza mpira kimiani wakati akijaribu kuuokoa.
Lionel Messi alichomoa goli hilo
dakika sita baadaye na kufanya matokeo kuwa Real Sociedad 1-1
Barcelona.
Lionel Messi akiachia shuti la guu lake la kushoto na kufunga goli la kusawazisha
Luis Suarez akiwa ameshika kichwa baada ya Barcelona kufungwa goli la kwanza
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni