Timu ya Arsenal imemaliza mwendo wa
sare tatu mfululizo baada ya Alexis Sanchez kufunga mara mbili na
Theo Walcott kufunga mara moja katika mchezo na Bournemouth na
matokeo kuwa magoli 3-1.
Katika mchezo huo Sanchez aliandika
goli la kwanza katika dakika ya 12 kufuatia makosa ya pasi ya nyuma
mbovu ya Steve Cook, hata hivyo goli hilo lilisawazishwa na Callum
Wilson kwa njia ya penati.
Arsenal nusura waongeze goli la pili
pale shuti la Sanchez lilipogonga mwamb, lakini badaye Walcott
alifunga goli kwa mpira wa kichwa akiunganisha mpira wa krosi ya
Monreal. Sanchez aliongeza goli la tatu akiunganisha krosi ya Olivier
Giroud.
Alexis Sanchez akiachia shuti lililomshinda kipa wa Bournemouth na kutinga wavuni
Theo Walcott akiangalia mpira wa kichwa alioupiga na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni