Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla Akiwa anamtunuku mmoja wa mwanafunzi wa shahada ya uzamini aliyejulikana kwa jina la Anna
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu fani za astashahada, shahada ya kwanza na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii katika chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru wakiwa wanajiself na naibu waziri mara baada ya mahafali hayo kumalizika
wanafunzi waliofanya vizuri zaidi shuleni hapo waliosimama nyuma wakiwa katika picha ya pamoja na naibu waziri pamoja na bodi ya chuo hicho
Naibu waziri akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mahafali kumalizika wa kwanza kulia ni Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki wakwanza kushoto ni kaimu mwenyekiti wa bodi ya taasisi hiyo Dr,Rosemarie Mwaipopo
wahitimu wakiwa katika nyuso za furaha Na Woinde Shizza,Arusha
Serikali inajipanga kuajiri maafisa ustawi wa maendeleo ya jamii 5,554 kwakipindi cha miaka mitano ili waweze kutoa huduma za maendeleo ya jamii kuanzia ngazi ya kata na vijiji kama ilivyokuwa kwa utawala wa awamu ya kwanza nchini
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla alipokuwa akihutubia katika mahafali ya sita katika fani za astashahada, shahada ya kwanza na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii katika chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru nje kidogo ya jiji la Arusha
Alisema kuwa serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa na idadi kubwa ya mabibi na mabwana maendeleo ya jamii kila kata hivyo ilisaidia kuwaletea maendeleo wananchi kwa haraka zaidi na kutoa ushauri wa miradi mbalimbali inayowazunguka wananchi haswa wa vijijini.
“katika serikali ya awamu ya kwanza maafisa ustawi wa jamii walikuwa wapo hadi vijijini unakuta bibi ustawi wa jamii na babu ustawi wa jamii kitu ambacho kwa kipindi cha nyuma hapa kilipotea kabisa sasa serikali hii ya awamu ya tano tunataka kurudisha icho kitu”alisema Kigwangala
Alivitaka vyuo mbalimbali vinavyofundishia kozi ya ustawi wa jamii kuakikisha wanaongeza idadi ya wataaalamu wanaosomea ustawi wa jamii ili kuweza kupunguaza tatizo hili kwani kwa sasaivi kadri siku zinavyozidi kwenda ndivo wanafunzi wanaosomea ustawi wa jamii wanapungua
“ kwasasa wataalamu katika sekta ya maendeleo ya jamii wameanza kupungua sana na ivyo kila chuo kinatakiwa kuongeza idadi ya wa wanafunzi ili kuendana na azima ya serikali ya kuwa na wataalamu wa maendeleo ya jamii kila wilaya , kata na hata kijiji.
Kigwangala alitoa wito kwa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuendela kutoa elimu yenye viwango bora na wazingatie katika mchakato wote wa utoaji mafunzo kuanzia kwenye udahili wa wanafunzi wenye sifa na vigezo ili kujenga jamii ya wasomi wenye tija katika Taifa letu.
" napia napenda kusema kuwa hao wamaafisa ustawi wa jamii wasome kabisa wakijua serikali itawaajiri sawa lakini wasitegemee watakaa ofisini tu au katika ofisi za halmashauri apana wajue kabisa wataenda kufanya kazi vijijini ili waweze kutambua matatizo ya wananchi na kuyatatua pamoja nakuvumbua miradi mbalimbali ya jamii itakayosaidia wananchi "alisema Kigwangala
Alisema Nchi itabadilika sana na kuwa na maendeleo ikiwa wanataaluma wa Nchi hii wataipenda Nchi yao kama ambavyo kila mtu ampendavyo mama yake nakujituma sana katika utendaji kazi utaendana na falsafa ya hapa kazi tu.
Kwa upande wake Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki akisoma hutuba wakati Mahafari hayo alisema kuwa pamoja na mikakati iliyopo ya kuboresha chuo hicho kwasasa chuo kimeanzisha kituo cha taifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho ya wanawake Nchini kituo ambacho kimeanzishwa kwa ushirikiano wa UNESCO na UNFPA pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kufanya tafiti za kina kwa masuala ya wanawake, jinsia, watoto wa kike ili kuwainua kiuchumi, kisiasa,kiutamaduni na kijamii na kuzitumia tafiti hizi kujadili katika kuandaa sera na kutoa maamuzi yanayojumuisha amsuala ya kijinsia katika kutekeleza sera mbalimbali hapa Nchini.
Wakwanza kushoto ni mkuu wa taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru Anatory Bunduki akiteta jambo na Naibu waziri Kigwangala
maandamano yakiwa yanaingia katika eneo la shule kwa ajili ya mahafalibaadhi ya walimu wakiwa katika maandamano hayo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni