Kinda Ben Woodburn amevunja rekodi
ya Michael Owen ya kuwa mchezaji kijana mno kuifungia Liverpool na
kuisaidia timu hiyo kuifunga Leeds United katika mchezo wa robo
fainali ya kombe la EFL.
Wenyeji Liverpool wakiwa katika
dimba la Anfield walipata goli lao la kwanza kupitia kwa mchezaji
mwenye asili ya Kenya Divock Origi akitumbukiza kimiani mpira wa
krosi ya winga wa kulia Trent Alexander-Arnold.
Liverpool walifanya matokeo ya
mchezo huo kumalizika kwa magoli 2-0, pale kinda Ben Woodburn
alipoandika historia mpya ya kuwa mchezaji kinda kuifungia goli
Liverpool akiwa na umri wa miaka 17.
Divock Origi akiifungia Liverpool goli la kwanza
Kinda Ben Woodburn akiachia shuti lililomshinda kipa wa Leeds United na kujaa wavuni



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni