Liverpool imefikisha michezo 11 ya
Ligi Kuu ya Uingereza iliyocheza bila ya kupoteza baada ya kuibuka na
ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Sunderland lakini huenda ikawa na
wakati mgumu bila mchezaji wao Philippe Coutinho aliyeondolewa
uwanjani kwa machela.
Mchezaji huyo raia wa Brazil
alitenguka enka yake wakati akikabiliana na Didier Ndong katika
dakika za mwisho za kipindi cha kwanza ambacho Liverpool ilikitawala
kwa asilimia 80 bila ya kufunga.
Hata hivyo Liverpool waliendelea
kushambulia lango la Sunderland na alikuwa Divock Origi aliyeingia
kuchukua nafasi ya Coutinho na kuifungia goli la kwanza na kisha
James Milner kufunga la pili kwa mkwaju wa penati wa dakika za
majeruhi.
Divock Origi akiachia shuti lililoenda na kujaa wavuni na kuifungia Liverpool goli la kwanza
Enka ya Philippe Coutinho ikiwa inaonekana kupinda baada ya kubambikiana na Didier Ndong
Philippe Coutinho akigugumia maumivu baada ya enka yake kuumia huku refa akiwa amemshika bega
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni