Cristiano Ronaldo ameiongoza Real
Madrid kupata ushindi dhidi ya Sporting Gijon katika dimba la
Bernabeu, baada ya kufunga magoli mawili yaliyomfanya kuongoza kwa
kufunga magoli mengi katika ligi ya La Liga.
Ronaldo amekuwa wa kwanza kufikisha
magoli 10 katika msimu huu katika ligi hiyo, na kwa magoli mawili ya
jana yalitosha kuinyima ushindi Sporting katika mchezo huo uliochezwa
huku mvua ikinyesha.
Kwa ushindi huo wa magoli 2-1
umeifanya Real Madrid kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba dhidi
ya timu ya Barcelona ambayo inashuka dimbani leo kucheza ugenini na
Real Sociedad.
Kinara wa magoli La liga Cristiano Ronaldo akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli
Kocha Zinedine Zidane akiwa anatoa maelezo kwa wachezaji wake bila ya kujali mvua inayomnyeshea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni