Chelsea imerejea kileleni mwa Ligi
Kuu ya Uingereza ikitokea nyuma baada ya kufungwa goli katika dimba
la Stamford Bridge, na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya
Tottenham.
Katika mchezo huo Tottenham
walionekana wakiwa vyema baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa
Ulaya kati kati ya wiki, na walikuwa wa kwanza kupachika goli kupitia
kwa Christian Eriksen.
Tottenham inayonolewa na Mauricio
Pochettino ilitawala kabisa mchezo huo hadi pale katika dakika za
mwisho za kipindi cha kwanza, Pedro aliposawazisha goli kwa mpira wa
shuti la kuzungusha uliojaa wavuni ukipitia katika kona ya juu ya
goli.
Chelsea iliendelea kupambana kiume
na alikuwa Victor Moses aliyefunga goli la pili, na kutibua rekodi ya
Tottenhma ya kutokufungwa katika Ligi Kuu ya Uingereza kwa msimu huu.
Pia amtokeo hayo yanaweka rekodi ya Tottehma kutoifunga Chelsea
nyumbani kwa michezo 30.
Cristian Eriksen akifunga goli la kwanza katika mchezo huo huku mabeki wawili wa Chelsea wakiwa chini
Pedro akijipinda kuachia shuti kali lililoenda kujaa wavuni na kuandika goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni