Sergio Aguero ametikisa nyavu mara
mbili wakati Manchester City ikitokea nyuma baada ya kufungwa goli
moja na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Burnley katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Wenyeji Burnley walikuwa wapate
penati, kabla ya kupata goli la kuongoza baada ya beki wa Manchester
City Nicolas Otamendi kuokoa mpira vibaya na kumfikia kiungo Dean
Marney aliyeachia shuti la yadi 25 na kujaa wavuni.
Manchester City walihangaika
kurejesha goli hilo na alikuwa Sergio Aguero aliyeudokoa wavuni mpira
baada ya mpira wa kona kumfikia. Goli hilo liliamsha ari kwa City
ambapo krosi ya Fernandinho ilimkuta Aguero na kufunga goli la pili.
Dean Marney akiwa ameachia shuti lililojaa wavuni na kuiandikia Burnley goli
Sergio Aguero akishangilia na mchezaji mwenzake baada ya kufunga goli la ushindi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni