JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti :
www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli,
amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Raul
Castro kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro
kilichotokea tarehe 25 Novemba, 2016.
Katika
Salamu hizo Rais Magufuli amesema;
"Nimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya
Cuba Mhe. Fidel Castro. Kwa niaba ya Serikali, Wananchi wa Tanzania
na kwa niaba yangu mwenyewe natoa pole nyingi kwako, familia,
Serikali ya Cuba na wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu.
Fidel
Castro alikuwa kiongozi shupavu wa karne, atakumbukwa kwa mchango
wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na pia kwa
misaada mikubwa aliyoitoa katika kuboresha huduma za kijamii kwa
wananchi.
Alikuwa
rafiki wa Tanzania na Afrika nzima, historia ya Tanzania na Afrika
haziwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro, hakika kifo chake sio
tu ni pigo kwa Cuba bali pia kwa Tanzania na Afrika.
Naungana
nawe na wananchi wa Cuba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, na
pia nakuombea kwa Mwenyezi Mungu wewe, familia na wananchi wote wa
Cuba muwe na nguvu, subira na ustahimilivu kutokana na kuondokewa na
mpendwa wenu."
Pia
Rais Magufuli amemuombea marehemu Fidel Castro apumzishwe mahali pema
peponi, Amina.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam
26
Novemba, 2016
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni