Borussia Dortmund na Legia Warsaw
zimeweka historia katika Ligi ya Mabigwa Ulaya kwa mchezo wao kuwa na
matokeo ya kufungwa magoli 12, yakiwa ni idadi kubwa ya magoli kuwahi
kutokea katika mchezo mmoja.
Dortmund inayonolewa na Thomas
Tuchel iliifunga Legia Warsaw magoli 8-4 katika mchezo ambao
utabakiwa kuwa wa kumbukumbu uliochezwa nchini Ujerumani.
Matokeo hayo yanaipiku rekodi ya
magoli 11 kufungwa katika mechi moja wakati Monaco ikiifunga
Deportivo La Coruna kwa magoli 8-3 mwaka 2003.
Katika mchezo wa jana magoli 7
yalifungwa ndani ya dakika 22 za mwanzo wa mchezo huo. Marco Reus
alifunga magoli matatu yaani hat-trick na Shinji Kagawa akifunga
magoli mawili.
Marco Reus akiwa ametumbukiza mpira kimiani
Oussmane Dembele licha ya kutegeneza magoli matatu alipachika goli moja
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni