Mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth
Bale itabidi asubiri kuona iwapo atakuwa mzima kuweza kucheza mchezo
wa El Clasico dhidi ya Barcelona baada ya kuumia jana.
Nyota huyo wa Wale, 27, alitoka
akichechemea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya walioshinda kwa
magoli 2-1 dhidi ya Sporting Lisbon akiwa ameumia enka.
Vinara hao wa ligi ya La Liga
wanaoongoza kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Barcelona wataenda Nou
Camp jumamosi ya Desemba 3.
Varane akiifungia Real Madrid goli la kwanza katika dakika ya 29
Karim Benzema akifunga kwa kichwa goli la ushindi kwa Real Madrid
Gareth Bale akiwa amelala chini akigugumia maumivu ya enka
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni