Timu ya Leicester City imeendeleza
mwenendo mzuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutinga hatua ya
mtoano baada ya kuifunga Club Brugge kwa magoli 2-1.
Katika mchezo huo Leicester City
ilikuwa inahitaji pointi moja tu kutinga hatua ya 16 bora lakini
ikapata pointi tatu zitakazo wahakikishia kumaliza wakiwa vinara
katika kundi G.
Shinji Okazaki alifunga goli safi la
kwanza akiunganisha krosi ya Christian Fuchs, huku Riyad Mahrez
akifunga goli la ushindi kwa shuti la penati, Jose Izquierdo alifunga
goli pekee la Club Brugge.
Mpira uliopigwa na Shinji Okazaki ukitinga wavuni na kuandika goli
Riyad Mahrez akifunga goli la pili la Leicester City kwa mkwaju wa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni