Jamii nchini Afrika Kusini
imemlalamikiwa vikali Mchungaji mmoja nchini humo ambaye anawapulizia
dawa ya mbu waumini wake wenye matatizo mbalimbali.
Akitumia ukurasa wake wa Facebook
Mchungaji huyo anayejiita Mtume Lethebo Rabalago, amedai kuwa dawa ya
mbu ya Doom inauwezo wa kufanya uponyaji.
Kampuni inayozalisha Doom imeonya
juu ya madhara ya kumpulizia mtu dawa hiyo na tume ya serikali
imewataka waumini waliodhurika kufungua malalamiko dhidi ya Mchungaji
huyo.
Hata hivyo Mchungaji huyo wa kanisa
la Mount Zion General Assembly katika mkoa wa Limpopo amejitetea
kuwa anatumia miujiza kutibu watu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni