Ijumaa, 18 Novemba 2016
MJUE MNYAMA TEMBO NA SIFA ZAKE
Na Pamela Mollel,Mikumi
Tembo ni mnyama kubwa kuliko wote lakini sio mrefu kama twiga,kuna aina mbili ya tembo.tembo w a bara la Afrika na bara la Asia
Ukitaka kujua tofauti zao wa bara la Afrika ni wakubwa ,na maskio yao yanamuonekano wa ramani ya bara la afrika lakini tembo bara la Asia wanamasikio madogo na pia wanaweza kufundishwa kulima na michezo mbalimbali
Akizungumza na waandishi wa habri kuhusu mnyama huyo (Tembo)Afisa wa shirika la Tanapa katika hifadhi ya Mikumi Abdalla Choma alisema kuwa Tembo hao wa wa bara la Afrika wapo katika makundi mawili,
1. Tembo wa msituni wanameno ambayo yamenyooka kwaajili ya kuwawezesha kupita katika msitu
2. Tembo wa Savana, meno yao yamepindapinda wanapenda kuishi katika familia moja wanaweza kuishi kwanzia wawili hadi 45 kwa familia
Alisema Tembo wauwezo mkubwa wa kusikia na wanakumbukumbu ya kutosha
Akizungumzia kuhusu uzazi wa tembo mzee Chuma alisema kuwa tembo wanauwezo wa kubeba mimba na kuzaa kwa miezi 18-20
Tembo huyo hunyonyesha motto wake kwa takribani miaka miwili hadi mitatu na motto wa tembo huyo akishafikisha miaka 15 huesabika ameshakuwa na kutakiwa kuondoka katika familia hiyo na kwenda kujitegemea
Tembo huishi kwa miaka 60-75 kwa sasa lakini miaka ya nyumba walikuwa na uwezo wa kuishi miaka 80-120 .
“Sababu za kuishi miaka michache kwa miaka hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi “alisema mzee Mchoma
CHAKULA CHA TEMBO
Anapenda kula matawi ya miti na nyasi za chini alafu anakula kwa maasaa 16 kati ya masaa 24. Kiasi cha chakula anachokula ni kati ya 150-300 kg kwa tembo mkubwa na hunywa maji kati ya lita 200 hadi 250
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni