Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha hilo. Picha na Muhidin Sufiani
Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha hilo. Picha na Muhidin Sufiani
Dk. Posi amebainisha katika Tamasha hilo kuwa, serikali ipo karibu na watu wenye ulemavu na kwamba sheria iliyopitishwa mwaka 2010, kuhusu watu wenye ulemavu imepitishwa na kwamba ni jukumu la jamii nzima kushirikiana katka kutoa haki sawa kwa wananchi wote wakiwemo walemavu.
Dk. Posi alifafanua kuwa, changamoto zinazowakabili walemavu hapa nchini ni nyingi lakini pia serikali inazitambua, inazichambua na inazifanyia kazi kwa kadri uwezo unapopatikana.
Kabla ya hotuba ya Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society, Fransis Kiwanga alifafanua kuwa, shirika analoliongoza kwa kutambua umuhimu wa kuwawezesha walemavu hapa nchini, liliona ni busara kuchangia kuwepo kwa tamasha hili na kwamba ni faraja kwa shirika hili kuona maisha na hali ya walemavu hapa nchini inabadilika.
“Tunaipongeza serikali kwa kazi kubwa inayofanya, tunaipongeza sana katika suala zima la kupinga rushwa, Tunaipongeza katika kuhakikisha kunakuwepo mabadiliko ya utendaji pamoja na utoaji huduma kwa wananchi,” Mkurugenzi huyo alisema na kuongeza kuwa, shirika lake kwa kutambua haki mbalimbali za walemavu na hali halisi ya maisha hapa nchini, linaiomba serikali kuhakikisha kuwa inakuwa karibu na watu wenye mahitaji maalum ili nao wajione kuwa ni raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu.
Tamasha hili linalounganisha wawakilishi wa watu wenye mahitaji maalum kutoka pane zote za Tanzania, linafanyika kwa siku mbili na likihusisha wawakilishi wapatao 150 kutoka katika mikoa yote nchini Tanzania na linafanyika hapa jijini Dar es Salaam kwa siku mbili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni