Serikali imesema kuwa Tanzania ina fursa nzuri katika uwekezaji wa huduma za kifedha na kuwavutia wawekezaji wa mataifa tofauti na malalamiko ambayo yamekuwa yakienezwa na baadhi ya taasisi hizo hapa nchini.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijazi
wakati wa ufunguzi wa tawi la jipya la Kariakoo la benki ya United Bank
Limited (UBL) Tanzana Limited.
Hivi kaibuni kulikuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya taasisi za kifedha na kutoa viashiria vya kufirisika, jambo ambali alisema, uzinduzi wa tawi la Kariakoo la benki ya UBL ni ishara tosha kuwa sekta ya uwekezaji wahuduma za kifedha hipo imara na kuendelea kuwavutia wawekezaji.
WaziriKijazi alisema kuwa uchumi wa Tanzania kwa sasa unakuwa na bodi ya
wakurugenzi wa benki ya UBL imevutiwa nayo na kuamua kuwekeza nchini.
Alisema kuwa benki hiyo kwa sasa imetumia jumla ya dola za Kimarekani
milioni 32 (Sh 67.2 bilioni) kutoa mikopo kwa wateja wake na huduma
nyingine
“Benki ya UBL Tanzania ilianza rasmi Mwezi Septemba mwaka 2013 na kufanikiwa kupata faida iliyopelekea kuzindua tawi linginehuku ikiwa na mipango ya kufungua matawi kadhaa katika mikoa ya Dodoma,Mwanza na Arusha, hii ni ishara tosha kuwa sekta ya huduma ya kifedha
Tanzania inakuwa na kupata maendeleo makubwa,” alisema Dk Kijazi.
Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa UBL Bw. Wajahat Husain alisema
kuwa wamefuraishwa na hali ya uwekezaji hapa nchini na kuamua kuwekeza,
ikiwa ni tawi la kwanza la benki hiyo kwa bara la Afrika.
Husain alisema kuwa wameichagua Tanzania kutokana kukuwa kwa uchumi, hali bora ya kisiasa, maliasili na huduma za bandari ya Dar es Salaam ambayo
ni kiungo cha wafanyabiashara, si kwa Tanzania tu, bali hata kwa nchi
sita jirani. Alisema kuwa kupanuka kwa mtandao wa benki hiyo kwa Dar es
Salaam kutaifanya benki hiyo kuwa kiungo muhimu cha masuala ya
kiuchumi.
“Tumefurahi kuwekeza hapa nchini, benki yetu ni miongoni mwa beki kubwa sana nchini Pakistani, tukiwa na matawi zaidi ya 1,300 na kutoa huduma wengi, tumevutiwa na hali ya uwekezaji hapa nchini na muda mfupi tuliowekeza, tumeona matunda yake na kuamua kupanua
wigo,” alisema Husain ambaye pia ni Mwenyekiti wa Benki hiyo nchini.
Alisemakuwa wapo tayari kwa soko la ushindani la hapa nchini na nyenzo yao
kubwa ni kutoa huduma za kisasa zenye ufanisi mkubwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni