.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 15 Novemba 2016

OSCAR PISTORIUS AHAMISHIWA KWENYE GEREZA LENYE MAZINGIRA BORA KWA WAFUNGWA WALEMAVU

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini aliyefungwa Oscar Pistorius amehamishiwa kwenye gereza lingine baada ya kuomba kufanyiwa hivyo.

Pistorius aliomba kuhamishiwa kwenye gereza la karibu la Atteridgeville, Idara ya Magereza ya Afrika Kusini imesema.

Gereza hilo lililopo nje ya Jiji la Pretoria, linamazingira mazuri kwa wafungwa walemavu. 

Pistorius anatumikia kifungo cha miaka sita kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni