Goli la kipindi cha kwanza la
Pierre-Emerick Aubameyang, limeipatia Borussia Dortmund ushindi dhidi
ya Bayern Munich katika mchezo huo wa miamba ya Ujerumani.
Aubameyang aliunganisha krosi ya
chini ya Mario Gotze iliyompita kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer,
na kuifanya Dortmund kuongoza katika dakika ya 11 ya mchezo huo.
Katika mchezo huo Frank Ribery
alifunga goli kwa kisigino katika kipindi cha pili lakini kibendera
kilinyooshwa juu kuashiria kuwa ameotea.
Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli pekee katika mchezo huo
Franck Ribery akifunga goli kwa kisigino ambalo lilikataliwa kutokana na kuotea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni