Pierre-Emerick Aubameyang amerejea
katika kikosi cha Borussia Dortmund kwa kishindo kwa kupachika magoli
manne, na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 5-2 dhidi
ya Hamburg.
Aubameyang, 27, raia wa Gabon
aliwekwa nje ya kikosi siku ya jumatano katika mchezo walioshinda wa
Ligi ya Mabingwa dhidi ya Sporting Lisbon kutokana na kuwepo kwa
tofauti za ndani ya klabu hiyo.

Aubameyang alirejeshwa kikosini na
kocha Thomas Tuchel jumamosi na kufunga hat-trick ndani ya dakika 23
za kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza goli la nne dakika chache tu
baada ya kuanza kipindi cha pili.
Katika mchezo huo pia Ousmane
Dembele aliifungia Borussia Dortmund goli, huku magoli ya Hamburg yote yakifungwa na Nicolai Muller.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni