Eden Hazard amefunga magoli mawili
wakati Chelsea ikitinga kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya
kuisambaratisha Everton kwa magoli 5-0.
Hazard aliifanya Chelsea iongoze kwa
kufunga goli la kwanza kwa shuti la chini, kabla ya Marcos Alonso
kuongeza la pili kwa goli tobo lililopita miguuni mwa Maarten
Stekelenburg.
Diego Costa aliongeza goli la tatu
kabla ya mapumziko na kisha Hazard kufunga tena kufumania nyavu,
ambapo Pedro alikamilisha karamu hiyo ya magoli kwa kufunga goli la
tano.
Eden Hazrad akijipinda na kuachia shuti ambalo lilijaa wavuni na kuandika goli
Diego Costa akishangilia goli baada ya kumpoteza golikipa maboyo na kufunga
Kocha wa Chelsea Antonio Conte akishangilia goli pamoja na wachezaji wake




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni