.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 5 Novemba 2016

TIMU YA MIDDLESBROUGH YAIBANA MANCHESTER CITY KATIKA DIMBA LA ETIHAD

Goli la mpira wa kichwa lililofungwa na Marten de Roon katika dakika za majeruhi limeinyima ushindi Manchester City katika dimba la nyumbani la Etihad, dhidi ya Middlesbrough.

Katika mchezo huo mshambuliaji Sergio Aguero aliifanya Manchester City kuwa mbele akitumbukiza kimiani krosi ya Kevin de Bruyne na kufikisha idadi ya magoli 150 akiwa na Manchester City.

Middlesbrough iliimarika baada ya mapumziko lakini Claudio Bravo aliokoa vyema mchomo wa Alvaro Negredo. Wakati kikosi cha Pep Guardiola kikiamini kinaibuka na ushindi De Roon alisawazisha kwa mpira wa kichwa krosi ya George Friend katika dakika ya 91.
                    Sergio Aguero akiangalia mpira alioupiga ukitinga wavuni na kuandi goli
   Marten de Roon akiwa ameruka juu kupiga mpira wa kichwa ulioandika goli la kusawazisha
          Mpira wa kichwa uliopigwa na Marten de Roon ukimshinda kipa Claudio Bravo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni