Sunderland wakiwa wamebakia 10
uwanjani wamepata ushindi wao wa kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza
katika msimu huu, wakati Jermain Defoe akifungwa goli la kipindi cha
pili kwa mkwaju wa penati dhidi ya Bournemouth.
Matokeo hayo yalikuwa muhimu kwa
timu hiyo inayojulikana pia kama Black Cats, ambayo ilionekana kuweka
presha kubwa kwa wapinzani wao Bournemouth na kujikuta wakimpoteza
Steven Pienaar dakika ya 59 aliyepewa kadi nyekundu.
Bournemouth walikuwa wa kwanza
kupata goli katika dakika ya 11 ya mchezo huo wakati Dan Gosling
alipounganisha mpira wa krosi uliopigwa na Adam Smith, na kufunga
goli lake la tatu katika msimu huu, ambalo lilisawazishwa na Anichebe
dakika ya 33.
Kipa wa Sunderland akiwa hana la kufanya baada ya Dan Gosling kufunga goli
Anichebe akiisawazishia Sunderland katika dakika ya 33 ya mchezo huo
Jermain Defoe akifunga kwa mkwaju wa penati na kufanya matokeo kuwa 2-1




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni