Shekiondo aliyefariki dunia juzi Novemba 20, mwaka huu kwenye Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam, alikuwa Makamu Mwenyekiti katika Kamati ya Muda ya Young Africans chini ya Mwenyekiti Tarimba Abbas na enzi zake Shekiondo anakumbukwa kutokana na ukarimu wake na uwajibikaji mzuri katika klabu.
Katika salamu hizo, Rais Malinzi amesema amepokea kwa masikitiko kifo cha Shekiondo kwa kuwa anafahamu vema utendaji wa Shekiondo wakati huo akiwa Kiongozi wa Young Africans Sports Club. Ni mtu wa mpira wa miguu ambaye amekuwa kwenye tasnia hii kwa muda mrefu wa maisha yake.
Kadhalika Rais Malinzi alituma salamu hizo kwa familia ya marehemu Shekiondo, ndugu, jamaa na marafiki ambayo kwa muda walikuwa wakimuuguza mpendwa wao na hivyo kutokana na kifo hicho, amewataka kuwa watulivu kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao.
Msiba wa marehemu Shekiondo ulikuwa nyumbani kwake, Ilala Mchikichini, Dar es Salaam ambako leo Novemba 22, mwaka huu umeagwa katika Kanisa la KKKT Lutheran, Temeke Wailes kabla ya kusafirishwa kwenda Korogwe kwa Shemsi mkoani Tanga kwa mazishi.
Bwana ametoa, bwana ametwaa. Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Shekiondo.
UAMUZI WA KAMATI YA SAA 72 YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA LIGI
Uchunguzi dhidi ya waamuzi Martin Saanya, Samuel Mpenzu (mechi ya Yanga Vs Simba), Thomas Mkombozi (mechi ya Coastal Union Vs KMC) na Rajab Mrope (mechi ya Mbeya City na Yanga) umekaribia kukamilika.
Hatua ya mwisho ya uchunguzi huo ni wao kufika mbele ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ambapo watahojiwa ili kutoa ufafanuzi katika masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika taarifa zao.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://www.tff.or.tz/news/685-uamuzi-wa-kamati-ya-saa-72-ya-uendeshaji-na-usimamizi-wa-ligi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni