Mshambuliaji wa Real Madrid,
Cristiano Ronaldo, amefunga magoli mawili na kukosa penati wakati
Ureno ikiifunga Latvia 4-1 katika mchezo wa kuwania kutinga michuano
ya kombe la dunia wa kundi B.
Cristiano Ronaldo alifunga goli lake
la kwanza kwa mkwaju wa penati lakini akakosa penati nyingine baada
ya mapumziko baada ya shuti lake kugonga mwamba.
Arturs Zjuzins aliisawazishia Latvia
kwa shuti la chini, lakini William Carvalho akaongeza la pili kwa
Ureno. Ronaldo alipachika goli la tatu na baadaye Bruno Alves
akakamilisha la nne.
Cristiano Ronaldo akiachia shuti na kufunga goli kwa mkwaju wa penati
William Carvalho akifunga goli la pili la Ureno kwa mpira wa kichwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni