Ubelgiji imejikita zaidi kileleni
kwa kundi H, baada ya kuichakaza Estonia kwa magoli 8-1 katika mchezo
wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia uliofanyika Jijini
Brussels.
Katika mchezo huo Dries Mertens na
Romelu Lukaku walitumia wavuni magoli mawili kila mmoja, ambapo pia
Thomas Meunier, Eden Hazard na Yannick Carrasco walifunga huku
Ragnar Klavan akijifunga.
Hata hivyo mchezo huo umeiacha
Chelesa na hofu ya kumkosa mchezaji wao Hazard, baada ya kutoka nje
ya uwanja katika dakika ya 74, ikionekana kuwa ameumia goti.
Mshambuliaji Romelu Lukaku akijaribu kuwatoka mabeki wa Estonia
Eden Hazard akiwajibika katika mechi hiyo ambayo hata hivyo hakuweza kumaliza baada ya kuumia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni