Kapteni wa timu ya taifa ya
Uingereza Wayne Rooney anataka kocha wa muda Gareth Southgate kupewa
moja kwa moja jukumu la kuinoa timu hiyo, kutokana na kuipatia
matokeo mazuri.
Rooney ametoa kauli hiyo wakati
Southgate akipata ushindi wa pili katika michezo mitatu aliyoiongoza
Uingereza, kwa kuifunga jana Scotland katika mchezo wa kuwania kufuzu
kombe la dunia.
Katika mchezo huo wa jana Uingereza
ilionekana kuwa imara zaidi ya Scotland na kuifunga kwa magoli 3-0,
magoli yaliyofungwa na Daniel Sturridge kwa mpira wa kichwa, na kisha
Adam Lallana kufunga la pili, Gary Cahill akafunga la tatu kwa kichwa
kufuatia mpira wa kona ya Rooney.
Daniel Sturrige akiwa chini akiangalia mpira wa kichwa alioupiga ukijaa wavuni
Gary Cahill akiwa ameupiga mpira kwa kichwa ambao ulimshinda kipa wa Scotland na kujaa wavuni



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni