Wachezaji Paul Pogba na Dimitri
Payet wamecheka na nyavu wakati Ufaransa ikiathimisha mwaka mmoja wa
mashambulizi la Paris kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Sweden,
katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia.
Kabla ya kuanza mchezo huo uwanja
mzima ulikaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka watu 130 wahanga wa
mashambulizi hayo yaliyotokea Jijini Paris Novemba 13, 2015. Emil
Forsberg aliifanya Sweden iongoze katika kipindi cha pili kwa goli la
mpira wa adhabu.
Paul Pogba akiuangalia mpira alioupiga kwa kichwa ukielekea kutinga wavuni
Dimitri Payet akipiga mpira ulioenda kujaa wavuni na kuiandikia Ufaransa goli la pili



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni