Mshambuliaji wa Poland Robert
Lewandoski anahitaji kufanyiwa matibabu baada ya flea (Flare) zilizorushwa na
mashabiki wa timu yake kulipuka karibu yake katika mchezo mkali wa
kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Romania.
Mshambuliaji huyo wa Beyern Munich
hakujeruhiwa lakini alionekana kupatwa na mshtuko na hofu kwa tukio
hilo lililotokea katika kipindi cha pili na kusababisha mechi hiyo
kusimamishwa kwa dakika tano.
Katika mchezo huo ambao Poland
waliibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Romania Kamil Grosiki
alifunga goli la jitihada binafsi dakika ya 11, huku Lewandoski
akifunga la pili katika dakika ya 82 na la tatu kwa mkwaju wa penati
dakika ya 90.
Robert Lewandoski akinyanyua mikono juu kulalamikia moto wa flea iliyorushwa karibu yake
Robert Lewandoski akiziba masikio baada ya flea iliyorushwa kulipuka
Robert Lewandoski akiwa anapatiwa matibabu huku akiziba masikio yake baada ya mlipuko wa flea




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni