Wayne Rooney ameweka rekodi ya kuwa
mchezaji wa Manchester United kuifungia magoli mengi timu yake katika
ligi ya Uropa baada ya kufunga jana katika mchezo na Feyenoord
walioibuka na ushindi wa magoli 4-0.
Kapteni huyo wa Red Devils alifunga
goli lake la 39 katika michuano ya ligi ya Uropa kwa kuunyanyua mpira
juu ya kipa Brad Jones akiunganisha pasi ya uhakika kutoka kwa Zlatan
Ibrahimovic.
Rooney pia alimtengenezea Juan Mata
goli la pili, na kisha baadaye kipa Jones akajifunga goli la tatu
akijaribu kuuokoa mpira uliompita tobo uliopigwa na Ibrahimovic,
kabla ya Jesse Lingard kufunga la nne dakika za majeruhi kwa mpira wa
shuti la kuzungusha.
Wayne Rooney akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Juan Mata akiteleza na kufunga goli la pili
Hii ndio hatari ya kucheza na mchezaji anayecheza Kung fu: Zlatan
Ibrahimovic akirusha teke la juu kuupiga mpira ambao hata hivyo aliukosa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni