Waendesha mashtaka wanashinikiza
kufungwa jela miaka 10 mchezaji wa zamani wa Barcelona Samuel Eto'o
kwa tuhuma za kukwepa kodi wakati akichezea klabu hiyo.
Waendesha mashtaka pia wanataka
Eto'o kulipa faini ya dola milioni 15.1 kwa makosa manne ya kukwepa
kodi, na kuikosesha mamlaka ya kodi ya Hispania dola milioni 4 katika
mwaka 2006-2009.
Kama hiyo haitoshi waendesha
mashtaka pia wanataka adhabu kama hiyo itolewe kwa muwakilishi wake
kwa wakati huo Jose Maria Mesalles Mata.
Samwel Eto'o akiwa na Lionel Messi wakati huo akichezea Barcelona
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni