Na.Abdulaziz Nachingwea.
MNADA wa tano wa korosho unaosimamiwa na kuratibiwa na chama kikuu cha ushirika cha RUNALI,umesitishwa kutokana na mgomo wa wasafirishaji wa zao hilo.
Meneja wa chama hicho,Christopher Mwaya,alithibitisha kusitishwa mnada huo,ambao ulitarajiwa kufanyika jumapili ya tarehe 13 mwezi huu.Meneja huyo ambae chama chake kinasimamia na kuratibu kazi za vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) vilivyopo katika wilaya za Nachingwea,Ruangwa na Liwale,Alisema mnada huo hautafanyika kufanyika kama ilivyotarajiwa.
Kutokana na kutopelekwa korosho kwenye ghala kuu kutoka kwenye maghala ya vyama vya msingi.Mwaya alisema hali hiyo imesababishwa na wasafirishaji wanaosafirisha zao hilo kutoka kwenye maghala ya vyama vya msingi kugoma kuendelea na kazi hiyo
"Mgomo wa wasafirishaji ulianza tarehe tisa mwezi huu,tulitarajia kuingiza kilo 99745000 ,hata hivyo hazikuletwa.Kwahiyo mnada hautafanyika kesho,"alisema Mwaya.
Meneja huyo alisema wafanyabiashara hao(wasafirishaji) wanadai kuwa bei wanazolipwa kwa kazi hiyo ni ndogo."Walikutana na mkuu wa wilaya wakazungumza wakaleta rate zao(viwango vya bei),hata hivyo baadhi ya vyama vya msingi vinataka vifanyike kwanza vikao na wakulima kabla ya kukubali mabadiliko na reti hazo,"alifafanua.
Mmoja wawasafirishaji,ambae hakutaka jina lake litajwe kwa madai ya kutopenda kujiingiza kwenye ugomvi na serikali,alikiri kuwa wameacha kusafirisha kutokana na baadhi ya vyama kukiuka makubaliano,na vingine vinataka viwalipe chini ya bei za msimu uliopita.
Mfanyabiashara huyo alisema nijambo lisilokubalika wakati thamani ya shilingi inashuka lakini wao walipwe chini ya bei za mwaka jana.Huku akibainisha kuwa bei wanazotakiwa walipwe zitawasababishia hasara."Mimi binafsi siwezi kufanya kazi ambayo itanisababishia hasara,kwenye biashara siasa ziwekwe pembeni,"alisema mfanyabiashara huyo Akizungumzia suala hilo,
mkuu wa wilaya ya Nachingwea,Rukia Muwango,alisema kulikuwa na kukosekana makubaliano baina ya wasafirishaji na vyama vya msingi,ambavyo ndivyo venye haki na jukumu la kusafirisha korosho za wakulima kutoka kwenye maghala ya vyama hivyo kwenda kwenye maghala maalum yanayotumika kuhifadhia na kuchukuliwa na wanunuzi.
Mkuu huyo wa wilaya,ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama(w),alisema suala hilo lilifikishwa ofini kwake na limeshugulikiwa kikamilifu.Bali kuna wafanyabiashara wenye tamaa baada ya kuona bei ya zao hilo ni mzuri mwaka huu.
Hata hivyo wapo wasafirishaji wanaendelea kusafirisha.Alisema lengo la serikali ni kuona wakulima wananufaika na kazi yao halali.Kwahiyo haiwezi kutishwa na watu wachache,wenyetamaa na wanaofanya kazi kwa mazoea." Mnada utafanyika jumatam ijayo baada ya kusitishwa wiki hii,wakulima wasiwe na hofu kila kitu kitakwenda vizuri,"alisema.
Tangu kuanza ununuzi wa zao hilo linazalishwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi na Mtwara,msimu wa 2016/2017,kwa minada minne iliyofanyika.Jumla ya kilo 10,170,438 zimeuzwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni